TUME KUKUTANA NA WADAU WA MIKOA YA GEITA NA TABORA

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania inatarajia kukutana na wadau kupitia mikutano yake miwili iliyopangwa kufanyika katika mikoa ya Geita na Tabora kuanzia tarehe 15-19 Sept 2014.

Katika mkoa wa Geita mkutano utafanyika wilaya ya Chato na kuwahusisha wadau kutoka kada mbalimbali na ule wa Tabora utafanyika katika wilaya ya Tabora Mjini.

Mikutano hiyo ni moja ya jitihada za Tume kujenga na kudumisha mahusiano mazuri na wadau wake kupitia mikutano na semina kwa nia ya kujenga uelewa wa masuala ya sheria na pia kupata maoni ya wadau namna ya kuboresha sheria.

Kwa taarifa hii Tume inawakaribisha wadau wake ili wapate fursa ya kusikia shughuliza Tume na kutoa maoni yao kuhusu  namna ya kuboresha Sheria nchini.

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania inalojukumu la kuelimisha umma kuhusu  maboresho mbalimbali ya Sheria kwa wadau wake. 

 

 

Powered by WordPress | Designed by: Premium WordPress Themes | Thanks to Themes Gallery, Bromoney and Wordpress Themes