Mikutano ya Wadau kuhusu utafiti wa Sheria zinazowalinda Walaji na Watumiaji Bidhaa

 

Tume ya Kurekebisha Sheria inafanya mapitioi ya sheria zinazowalinda walaji na watumiaji bidhaa kwa nia ya kuziboresha ili kuhakikisha kuwa sheria hizo zinaenda na wakati kwa kulinda haki za walaji na watumiaji bidhaa.

Katika kuhakikisha kuwa wadau wanashiriki ipasavyo katika mapitio haya, Tume inatarajia kufanya utafiti wa sheria husika kwa awamu mbili.  Awamu ya Kwanza itajumuisha  Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Mara, Mwanza na Shinyanga. Tume itaanda mikutano ya wadau mbalimbali  ambao watapata nafasi ya kutoa maoni yao. Mikutano hiyo imepangwa kufanyika kuanzia tarehe 12-20 Oktoba, 2015.  Awamu ya Pili itafanyika siku za baadae  katika mikoa mingine ya Tanzania Bara. Wadau mnakaribishwa kushirikiana na Tume kwa kutoa maoni kwa njia ya barua pepe na barua. Maoni yenu ni muhimu sana kwani yatasaidia kuboresha sheria zilizopo. Ratiba ya Mikutano ni kama ifuatavyo;

 

Tarehe 13/10/2015 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara

Tarehe 16/10/2015 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza

Tarehe 19/10/2015 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga

Powered by WordPress | Designed by: Premium WordPress Themes | Thanks to Themes Gallery, Bromoney and Wordpress Themes