Tume Kufanya Kikao cha Baraza la WafanyakaziTarehe 30-31/03/2015
Tume ya Kurekebisha Sheria itafanya kikao chake cha Baraza la Wafanyakazi mkoani Dar es Salaam kuanzia tarehe 30-31 Machi 2015 katika Ukumbi wa Tumesheria.
Kikao hicho kinatarajiwa kufunguliwa na Mwenyekiti wa Tume Jaji Aloysius Mujulizi. Mkutano huu wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ni Mkutano wa kumi na mbili (12). TUMESHERIA katika kipindi chote, imehakikisha kuwa inatekeleza wajibu wake ipasavyo kwa kuhakikisha vikao vyote vya Kisheria Agizo la Rais Na.1 la Mwaka 1970 pamoja na Sheria mbalimbali zinazohusiana na masuala ya Ajira na Mahusiano Kazini Mkataba wa Uanzishaji wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika tarehe 05/03/2010.
Katika kikao hicho, Mada kuu iliyopangwa kujadiliwa ni Mwenendo wa Bajeti ya Tume 2014/2015 na Bajeti ya mwaka 2015/2016. Aidha, hoja mbalimbali za Watumishi zitajadiliwa.